Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Mkuu wa Kiwanda cha Viatu Gereza Kuu Karanga, Moshi, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Hezron Nganoga alipotembelea kiwanda hicho kukagua maboresho ya ufungaji wa mashine mpya za kutengenezea viatu vya aina mbalimbali ikiwemo buti zinazotumiwa na Majeshi ya Ulinzi na Usalama hapa nchini leo Agosti 1, 2018. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiangalia mtambo maalum wa kukata ngozi zinazotumika kutengenezea viatu. Mtambo huu ni mpya na ni sehemu ya maboresho katika kiwanda hicho.
Mtaalam kutoka nchini Italia akijaribisha mashine mpya ambazo zimefungwa katika Kiwanda hiki cha uzalishaji wa viatu cha Gereza Kuu Karanga(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike.
Maofisa Wataalam wa Jeshi la Magereza wakiendelea na majaribio ya mashine mpya katika mradi wa ubia uliokuwa mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF na Jeshi la Magereza.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiangalia buti la jeshi ambalo limetengenezwa kiwandani hapo. Wengine wakiangalia viatu hivyo ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa uliokuwa mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF, Hosea Kashimba(wa pili kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Onesmo Buswelu.
Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche (wa pili kulia) akionesha eneo la uwekezaji wa kiwanda kipya katika awamu ya pili ya mradi wa kiwanda cha viatu chini ya Kampuni ya Kiwanda cha viatu Karanga (wa pili kushoto) ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Viwanda vya ngozi – Gereza Kuu Karanga, Bw. Masoud Omary (wa tatu kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).
Post A Comment: