Katibu wa Umoja wa Vijana wa Ccm UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Comrade Hussein Egobano amefanya ziara katika Tawi la Imalilo kata ya Kitangili na kukutana na Vijana wa UVCCM wa Tawi ilo.

Pamoja na mambo mengi katibu amezungumza na vijana juu ya Matumizi ya Nguvu zao wakiwa bado ni vijana.

Katibu aliwahasa vijana,  huu  ndio wakati wetu vijana kuchangamkia fursa zilizoko katika maeneo yetu na wenye Elimu ni wakati wao kuitumia Elimu yao vizuri ili kujikwamua kiuchumi katibu aliendelea kusema itafikia wakati vijana wenzangu hizi nguvu tulizonazo leo hatutokuwanazo tena kwahiyo ninawahasa tujitaidi kufanya kazi kwa bidii ili tujikwamue kiuchumi.

Pia katibu alisisitiza vijana wa UVCCM tuendelee kuwa na upendo kwa chama chetu na serikali yetu kwa mnaona namna ambavyo Mwenyekiti wetu wa chama anajitaidi kufanya kazi kwahiyo nasi pia tuendelee kuchapa kazi kwa kufanya hivyo tutakuwa tumemuunga mkono Mheshimiwa Raisi wetu na mwenyekiti wa CCM .

Vijana ni nguvu kazi ya Taifa tukilala sasa na Taifa litalala kwahiyo tuamke tukafanye kazi.

Pia katibu aliwataka viongozi wa Jumuiya matawini kufanya kazi kwa mujibu wa kanuni kwani kumekuwepo na wimbi kubwa la viongozi wa Jumuiya yetu kutokutimiza majukumu yao ipaswavyo na kupelekea kuiua taswira nzuri ya Jumuiya yetu , katibu aliongezea kwa kusema kuwa hayuko tayari kumvumilia kiongozi ambae ashirikiani na vijana anaowaongoza katika matatiyo yao. Alisema hawa vijana tusiposhirikiana nao leo katika yanayoyataka kesho hatutoweza kuwaomba kura kwahiyo muda ni sasa.

Pia katibu aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi wakati utakapofika kugombea nafasi mbalimbali za uwakirishi wa wananchi katika vyombo vya Dola.

*Imetolewa na*
*Ofisi ya UVCM wilaya*
*Shinyanga Mjini*

#TUKUTANE KAZINI#
Share To:

msumbanews

Post A Comment: