KAMATI Kuu Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) leo tarehe 14 Agosti, 2018 imeketi jijini Dar es Salaam na kufanya uteuzi wa wagombea watatu katika majimbo ya Monduli, Ukonga na Korogwe Vijijini.

Kamati hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk. John Magufuli.

Kamati hiyo imemteua Julius Karanga kugombea jimbo la Monduli, Mwita Waitara ameteuliwa kugombea Ukonga na Timotheo Mzava ameteuliwa kugombea Korogwe Vijijini.

Katika hatua nyingine, kamati hiyo imewashukuru watanzania wote waliojitokeza kushiriki katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Buyungu na kata 77 na kukipa dhamana CCM na wagombea wake kwa kuwawezesha kushinda kwa asilimia mia.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: