Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula hivi leo amekabidhi mifuko 50 ya Saruji katika Hospital ya wilaya ya Nyamagana Butimba msaada kutoka kwa mdau wa maendeleo Mwanza Huduma. Mhe Mabula amesema Saruji hiyo inathamani shillingi 875,000 isaidie ujenzi wa uzio ili kuweka mazingira salama ya hospitali.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wilaya ya Nyamagana Dkt Kajiru Eliamani amemshukuru Mhe Mabula kwa jitihada zake za uboreshaji miundombinu ya hospitali, amemhakikishia msaada kujenga uzio wa hospitali hiyo kama ilivyokusudiwa.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Post A Comment: