Msanii wa Bongo Fleva, Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amerudishwa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ kwa ajili ya matibabu baada ya hali yake kuendelea kutokuwa vizuri licha kutolewa hospitalini huko siku chache zilizopita.
Dimpoz ambaye miezi miwili iliyopita alifanyiwa upasuaji mkubwa wa koo nchini Afrika Kusini, hali yake imekua haiimariki ipasavyo jambo lililosababisha kupandishwa ndege na kurudishwa tena huko kendelea na matibabu zaidi.
Tokea June 15,2018 Ommy Dimpoz hajaongea chochote wala kupost chochote kupitia ukurasa wake wa instagram zaidi ya vyombo vya habari kupata taarifa kutoka kwa Manager wa Ali Kiba ambaye ni Seven Mosha na kusema kuwa Ommy alikuwa akiendelea vizuri
Kupitia ukurasa wa instagram wa Madee Ali amempost Ommy Dimpoz na kuandika caption inayoonyesha kuwa hali ya Ommy Dimpoz sio nzuri hivyo anahitaji maombi kutoka kwa mashabiki.
Post A Comment: