Na. Vero Ignatus Arusha.
Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imewataka wananchi kufahamu wajibu na haki zao wanazostahili kupata kutoka kwenye mitandao inayotoa huduma za mawasiliano sambamba na kutambua wajibu walionao kama watumiaji wa huduma za mawasiliano
Kaimu mkuu wa Kanda ya kaskazini Francis Msungu amesema kuwa mamlaka inatoa elimu kwa wananchi kuzijua haki zao kutokana na mabadiliko yanayotokea ni mengi ya sayansi na teknolojia pamoja na maendeleo ya matumizi ya vifaa vya mawasiliano katika mitandao ya simu.
Amesema kwa sasa kumezuka wimbi la utapeli kupitia simu za mikononi, hivyo wananchi wametakiwa kuwa na tahadhari kubwa, wasikubali kurubuniwa katika vitu ambavyowanafahamuhawajashiriki Usitekeleze maagizo yeyote yahusuyo fedha kwa ujumbe wa maandishi,
"Mfano unatumiwa ujumbe kuwa umeshinda bahati na sibu katika
Mashindano ambayo hujashiriki, ukipokea ujumbe umetumiwa pesa na mtu usiyemfahamu usizitoe fedha hizo, hadi uthibitishe ya kwamba zimetumwa kwa nia nzuri"
Amewataka wananchi mara waonapo fedha imetumwa kwenye mitandao yao na aliyezituma bado hajafahamika, ni vyema wakawa na subira hadi watakapo hakikisha zimetumwa kwa nia njema ili wasiingie kwenye matatizo.
"Watu huwa wanakosea pia yamkini zilitumwa kwa bahati mbaya, ukiwahi kuzitoa nawe unahesabika unaiba. "alisema
Amewataka watumiaji wa simu za mkononi kufahamu kuwa zipo tahadhari za kuchukuliwa ikiwepo kusajili namba kwa majina kamili ya muhusika kwani ni takwa la kisheria, bila kusahau kwamba kila taarifa zinazoyolewa wakati wa usajili ziwe za sahihi.
Taarifa zako zikiwa za uongo hilo nikosa kisheria utapata adhabu ya kifungo au kulipa shilingi milioni 3 au vyote kwa pamoja.
Ameshauri kwamba yeyote akipoteza simu au kadi atoe taarifa kwa jeshi la polisi na kwa mtoa huduma, samba na kuchukua tahadhari mara uokotapo simu au kadi ya simu utoe taarifa kwa usalama wako zaidi
Wananchi wote wanaotembelea maonyesho 25 ya kilimo na sherehe za nanenane kanda ya kaskazini mwaka 2018 wanashauriwa kutembelea banda la TCRA ili waweze kupata elimu zaidi ya mawasiliano.
Post A Comment: