Na Magdalena Kashindye
Gari
la Mbunge wa CHADEMA Lucy Magereri lenye namba za usajili T l348 CSR
limepata ajali eneo la Issuna wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambapo
Dereva aliyefahamika kwa jina la Thomas Maro amepoteza maisha papo hapo.
Ajali
hiyo imetoka jana Agosti 9 ambapo ndani ya gari hiyo alikuwepo dereva
mwenyewe kwani alikuwa analitoa gari hilo Dodoma kulipeleka Shinyanga
ndipo lilipogongana na Fuso lililokuwa linatoka Singida kwenda Dar es
Salaam.
Dereva wa Fuso amepata majeraha madogo madogo huku mwili wa marehemu ukihifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.
Akithibitisha
kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert
Njewike amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Fuso kuendesha gari
upande ambao sio wake, na sasa amekamatwa yupo kituo cha Polisi kwa
ajili ya mahojiano.
Post A Comment: