Waziri wa Maliasiali na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akifanya mazoezi ya kutembea katika viunga vya Upanga Mashariki Jijini Dar es Salaam jana usiku ambapo alitembea umbali wa Kilometa nne. Wengine ni wasaidizi wake (Kulia) ni Katibu wa Waziri Ephraim Mwangomo na kushoto Ramadhan Magumba.
Waziri wa Maliasiali na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipanda ngazi jingo jipya la MOI lenye gorofa 6, jana usiku akirejea kwenye Wodi yake anapopatiwa matibabu. Wengine ni Wasaidizi wake (kushoto) ni Katibu wa Waziri Ephraim Mwangomo.
PICHA NA ANDREW CHALE
NA ANDREW CHALE, DAR

HALI ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla anayepatiwa matibabu na Madaktari Bingwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu, Ubongo na Uti wa Mgongo Muhimbili (MOI), imeendelea kuimarika siku hadi siku ambapo kwa sasa ameweza kufanya mazoezi ya kutembea umbali wa Kilometa 4, kwa kutumia muda wa saa moja na dakika 23.

Dkt. Kigwangalla ameweza kufanya zoezi hilo jana jioni kutembea umbali huo wa Kilometa 4 na kisha kupanda jengo la MOI kwa kutumia ngazi kutoka chini mpaka gorofa ya Sita.

“Kwa sasa naendelea vizuri. Tofauti na awali nilipokuwa natembea umbali mdogo kutoka Wodi ya Mwaisela nilipokuwa nimelazwa na kutembea mpaka getini la kuingilia Hospitali hii ya Muhimbili. Kwa sasa natembea umbali mrefu zaidi, nilianza na Kilometa moja, nikaongeza kilometa moja na nusu na baadae mbili… Lakini nikaona leo niongeze zaidi na kuweza kumaliza Kilometa hizi nne.

Mazoezi haya ya kutembea yananisaidia kuimarisha zaidi mapafu. Ila kwa sasa bado nashughulikia mkono pekee” Alieleza Dkt. Kigwangalla.

Dkt. Kigwangalla uanza kufanya mazoezi hayo kila siku kuanzia majira ya jioni kwa lengo la kiafya pamoja na tiba kwa hali yake hiyoambayo kwa sasa akiendelea na matibabu.

Kwa upande wa Madaktari wa MOI wamebainisha kuwa licha ya kuendelea vizuri, bado wanafuatilia kwa ukaribu hali ya afya yake hadi watakapojiridhisha ndipo watamruhusu kurejea nyumbani kuendelea na majukumu yake.

Dkt. Kigwangalla aliletwa MOI tangu Agosti 12, mwaka huu na kufanyiwa upasuaji wa mkono wake ambao ulivunjika kutokana na ajali aliyoipata Agosti 4, akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Manyara.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: