Diaomond Platnumz na Mameneja wake wawili, Babu Tale na Sallam wametinga BASATA kuitikia wito wa baraza hilo kuhusu malalamiko ya msanii wa muziki Rich Mavoko aliyedai kuwa mkataba wake na WCB umekaa kinyonyaji.

Akizungumzia hilo mmoja wa meneja wa Diamond, Sallam Sharraf, amesema waliitwa na Basata na sasa wapo katika mazungumzo.

Sallam ambaye hakuwa tayari kuliongelea suala hilo kiundani, amesema ni vyema watu wakasubiria yatakayoamuliwa huko, ambapo wanaamini Basata itauambia umma nini kilichoafikiwa badala ya wao  kuwa wasemaji.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: