Waumini wa Dini ya Kislamu Wilayani Hai wamemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambae pia ni Mzaliwa wa Wilaya ya Hai Kwa Kitendo chake cha Kukubali kuufanyia Ukarabati Msikiti wa Lyamungo Sinde Kwa kuweka Mabati mapya yote ya Jengo la msikiti ,pamoja na kuweka Sealing Board ndani , na ukarabati Mwingine Mdogo 

Akizungumza Kwa Niaba ya Viongozi wa Bakwata Wilaya ya Hai,Ramadhani Matinga ambae ni Mwenyekiti wa ZAWIA ya Lyamungo Sinde,amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kujitolea kwake,katika kuhakikisha mambo ya kijamii yanakwenda sambamba na maendeleo.
 
 Mbali na Kumshukuru Mhe Muro Kwa kukubali Kubeba Jukumu la Kukarabati Msikiti huo,amebainisa kuwa hawajawai kumuona Kiongozi Mkuu wa Serikali Kuanzia ngazi ya Kijiji, kata, wilaya na Mkoa na Hata Mbunge Pamoja na Taifa ambae ameingia katika Msikiti huo Isipokuwa Dc Muro,aidha wamemhakikishia kumpa Ushirikiano pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe Lengai Ole Sabaya Kutokana na Jitihada walizoonesha katika Kuwatumikia wananchi pasipo ubaguzi

Katika tukio Hilo Pia Mhe Muro alitoa Zawadi ya Mabox ya Tende Kwa Waumini wa Msikiti wa Lyamungo Sinde pamoja na kina mama wa Kware Wilaya ya Hai
DC Muro pichani kati akiwakaribisha badhi ya Waumini wa Msikiti wa Lyamungo Sinde kupata chakula kwa pamoja3
DC Muro akikabidh zawadi ya Mabox ya Tende Kwa Waumini wa Msikiti wa Lyamungo Sinde pamoja na kina mama wa Kware Wilaya ya Hai.1
3S
DC Muro akishiriki sala pamoja na Waumini wa Msikiti wa Lyamungo Sinde
Share To:

msumbanews

Post A Comment: