Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Mh. Jerry Muro, amefungua mkutano wa wabobezi wa utafiti katika ukanda wa Africa Mashariki '' The Eastern Africa Research and Innovation Management Association, Tanzania Chapter, mapema hii leo.

Dc Muro amemuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Arusha. Mh. Mrisho Gambo. Mkuu wa Wilaya amewapongeza Watafiti kwa Ubunifu wa kuwa na Jukwaa la Pamoja kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabiri wananchi wa jumuia ya Africa ya Mashariki.

Pia amewaeleza juhudi mbali mbali ambazo zinafanywa na Serikali yaTanzania za kuwezesha taasisi za kitafiti na za Elimu ya juu katika utafiti.

Ameeleza kuwa serikali inasubiria kupata mrejesho juu ya changamoto mbali mbali zitakazo bainishwa na wataalam hao ili kuendelea kutoa ushirikiano stahiki katika kuzifanyia kazi changamoto hizo. Mh. Jerry Muro, ameipongeza Taasisi ya Sayansi na Technolojia ya Nelson Mandela, iliyoko Tengeru, Arusha kwa kuonesha mfano mzuri wa tafiti zinazogusa maisha ya watu na viwanda na kusema kuwa kazi kubwa iliyobakia ni kushirikiana katika kuzifikisha kwa jamii na viwanda.





Share To:

msumbanews

Post A Comment: