Ndg. Charles Loiyandoi Nnko ,ambaye ni mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) aibuka mshindi wa uchaguzi mdogo Wa   Diwani Kata ya Songoro uliofanyika leo .
Ushindi huo ni mara baada ya msimamizi  msaidizi wa uchaguzi Kata ya Songoro Ndekirwa Mbise kumtangaza Charles Loiyandoi Nnko kuwa mshindi  kwa kupata  kura  4018 kati ya kura   zilizopigwa 4296 sawa na asilimia 93 huku mpizani wake Ndg.Goodluck Wilfred Nanyaro  ambaye ni mgombea kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kupata kura 278 sawa na asilimia 7,kura zilizoharibika ni kura 18.
Msimamizi huyo wa uchaguzi Kata  ya Songoro  amesema uchaguzi huo umefanyika kwa amani na utulivu  kwani wapiga kura wote waliofika kwenye vituo vya kupigia kura walipiga kura.    
Pia ameongeza kuwa zipo sintofahamu zilizojitokeza ambazo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi hazikuvuruga uchaguzi huo,akitaja mojawapo ni mawakala watokanao na  chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kuondoka katika vituo vyote 14 vya kupiga kura majira ya saa 5:45 asubuhi .
"Uchaguzi ulianza saa 1:00 asubuhi na kukamilika saa 10:00jioni hivyo mawakala wa CHADEMA walishiriki uchaguzi huo kwa zaidi ya masaa matano"ameeleza Mbise.
Kwa mujibu wa daftari la kupiga kura  la mwaka 2015 idadi ya wapiga  Kata ya Songoro ilipaswa kuwa 5690
Share To:

msumbanews

Post A Comment: