Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NIC Tanzania Mick Karima akizindua huduma ya kadi yake ya kwanza ya Visa Debit leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NIC Tanzania Mick Karima akimkabidhi mteja wao mfano wa kadi ya visa Debit iliyozinduliwa na Benki hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya NIC Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya zoezi hilo la uzinduzi wa kadi mpya ya Visa Debit kumalizika leo Jijini Dar es Salaam.

Na Leandra Gabriel, 

BENKI ya NIC imezindua kadi yake kwa mara ya kwanza kabisa ya Visa Debit iliyopewa jina la "Move" itakayowapa wateja wake njia rahisi na haraka zaidi katika kufanya malipo popote ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika ufunguzi huo Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Mick Karima ameeleza kuwa uzinduzi huo unaashiria hatua muhimu sana kwa benki yao na wanaendela kutoa huduma mbalimbali kwa wateja  zitakazoboresha maisha yao.

Aidha amesema kuwa benki hiyo inaendelea kutafuta ufumbuzi wa kuwaboreshea wateja matumizi ya huduma zao kwa kwenda mbele na kuwa wabunifu zaidi.

Pia ameeleza kuwa watanzania wengi wameonesha hamasa ya malipo ya kidigitali hivyo watahakikisha huduma hizo za kufanya malipo kwa njia ya mtandao zinawafikia wateja wao  na wana malengo makubwa mbeleni katika kujenga uchumi wa nchi hasa kwa  kwa kuzingatia sera ya nchi kwa sasa inayohamasisha na kuongeza kasi ua ukuaji wa malipo kwa njia ya kadi.

Naye Mkuu wa kitengo cha fedha na manunuzi wa benki hiyo Msafiri Kibebeti ameeleza kuwa lengo la uzinduzi wa kadi hiyo ni pamoja na kurahisisha na kuwawezesha wateja wao kufanya huduma (miamala) na hii yote ni katika kutimiza matakwa ya wateja na kutimiza azma ya serikali ya kujenga Tanzania ya viwanda.

Kibebeti amesema kuwa wapo imara na wamejizatiti kufanya kazi na wapo katika hatua za mwisho katika kufungua matawi katika Mikoa ya Dodoma na Zanzibar.

Benki ya NIC ilinunua hisa katika benki ya ya Savings and Finance Commercial Bank Group Tanzania na kuibadili chapa na kuwa benki  NIC  Tanzania na hadi sasa imezindua huduma kadhaa za kidigitali kwa lengo la kuwasaidia  wafanya biashara wadogo wadogo na hadi sasa wana matawi matano katika Mikoa ya Arusha, Mwanza(matawi 3,) na Dar es salaam matawi 3 (Ohio, Samora na Kariakoo.)
Share To:

msumbanews

Post A Comment: