NA TIGANYA VINCENT
Mkazi wa Kijiji cha Ikongoro wilayani Uyui Said Ramadhan ambaye alimuua mkewe Mwajuma Hussein kwa kumpiga risasi
kutokana na kile kilichodiwa wivu wa mapenzi na kisha kukimbia amekutwa amejiua kwa kujinyonga juu ya mti.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Emmanuel Nley kwa vyombo vya habari imesema kuwa matukio hayo yametokea Agosti 21 mwaka huu.

Alisema kuwa Ramadhani ambaye alikimbilia porini baada ya kutenda tukio la mauaji ya mkewe akiwa na bunduki aina ya gobore alikutwa amekufa kwa kujinyonga huku silaha hiyo ikiwa pembeni.

Kamanda Nley alisema kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kwani kabla Ramadahi ambaye sasa ni marehemu hajamuoa Mwajuma naye Marehemu alikuwa ameolewa na Jumanne Malawiro ambaye walizaa naye watoto wawili.

Alisema kuwa marehemu Ramadhan alihisi kuwa uenda mkewe bado ana mahusiano ya kimapenzi na mzazi mwenzie huyo ndipo akaamua kumuua na kisha yeye kujiua.

Katika tukio jingine Polisi wanamshikilia mkazi wa kijiji cha kombe wilayani Kaliua Chiga Lutumbiga kwa tuhuma ya kumpiga na kumuua mkewe Mwanza Kushema na kisha kutelekeza mwili wake katika msitu wa hifadhi ya Usawima.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 21 mwaka huu kwenye msitu wa Isawima kitongoji cha Kombe kata ya Igagala mwili wa mwanamke huyo uliokotwa ukiwa na majeraha kichwani na sehemu mbali mbali za mwili.

Kamanda Nley alisema kuwa katika ufuatiliaji imegundulika kuwa kabla ya kifo hicho marehemu alitumwa kufuata mahitaji kijiji cha Ugasa na alipochelewa kurudi nyumbani mumewe alimfuatilia na kumkuta njiani akirudi ndipo akampiga nakumwacha porini akiwa uchi.


Aliongeza kuwa mtuhumiwa baada ya kufika nyumbani alipiga kelele za kuomba msaada kwa wananchi wamsaidie kumtafuta mkewe ambaye walimkuta amekufa hapo msituni akiwa uchi huku akiwa na majeraha.
Share To:

Anonymous

Post A Comment: