Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipokea zawadi ya Mbuzi iliyotolewa na Askari wa kike wa Wilaya ya Serengeti baada ya kuzungumza na Maofisa, Wakaguzi na Askari wa Wilaya hiyo wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara ACP Juma Ndaki .
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akifurahia ngoma na kikundi cha utamaduni cha Kijiji cha Rubanda Wilayani Serengeti wakati alipofika kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi. (Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Rubanda Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi. (Picha na Jeshi la Polisi) 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima wakati alipofika ofisini kwake na kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Nurdin Babu wakati alipofika ofisini kwake na kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: