KUFUATIA hukumu iliyomkumba msanii Wema Sepetu ya mwaka mmoja jela au kulipa ya Tsh. Milioni 2, kwa makosa mawili ya kutumia madawa ya kulevya na kukutwa na madawa hayo nyumbani kwake, msanii huyo amelipa faini hiyo mahakamani hivyo hatotumikia kifungo hicho.

Hayo yameelezwa leo nje ya lango la Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar na Wakili wa Wema, Albert Msando ambaye amesema Wema hatotumikia kifungo hicho kwani tayari wameshafanya taratibu za kulipa faini ya milioni mbili kama mahakama ilivyoamuru.

Aidha, Msando amewataka wasanii kutojihusisha na madawa ya kulevya huku akisema kwamba Wema atakuwa balozi mzuri wa kuhimiza vijana na wasanii wenzake kuachana au kutokujiingiza kwenye  matumizi ya dawa za kulevya.

Pia amesema kwamba, kesi ya Wema imekuwa ndefu kwa sababu hakukubari mapema iwapo anatumia madawa ya kulevya kama ilivyokuwa kwa wasnii wenzake wakiwemo TID na Petit Man.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: