Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mkoa wa Kigoma (KUWASA), Simon Lupuga baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wake.
Mbarawa amefikia hatua hiyo baada ya malalamiko ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga kuwa mamlaka hiyo, Bonde la Mto Tanganyika na wahandisi wa maji hawatimizi majukumu katika nafasi zao kutokana na kufanya kazi kwa mazoea.
Vile vile, Waziri Mbarawa amesema atamuagiza Katibu Mkuu kuandika barua ya uhamisho wa Mkurugenzi huyo kurejeshwa Dar es Salaam kuanzia leo.
Post A Comment: