Waziri wa Ardhi William Lukuvi ameagiza kwanzia sasa hivi ni marufuku makampuni yote yanayojishughulisha na masuala ya upimaji wa ardhi kutoza zaidi ya shilingi laki mbili na nusu kwa kiwanja na anayeona hawezi kufanya kwa gharama hiyo bora aache.

Lukuvi ameyasema hayo alipokutana na wapimaji wa Ardhi na watendaji wa serikali za mitaa wa maeneo ambayo zoezi la urasimishaji ardhi limeanza kufanyika.

Reni Chiwa ni mmoja ya wapimaji ambao wanafanya kazi hiyo katika mitaa mbalimbali ukiwemio mtaa wa mshikamanoo magari saba Mbezi jijini Dar es Salaam ambaye anasema zoezi hilo linakwenda vyema ila jambo la msingi na kuhakisha upimaji ukimalika huduma muhimu za kijamii zinaweza kupataikana kupitia Ramia Naye watson Mwakalila amesema wizara inafanya kazi nzuri na kama mpango huo wa kurasimisha ardhi utatumika vyema utasaidia watu wengi kupata hati zao mapema.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: