Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema hatasita kufuta makanisa au misikiti inayoshindwa kutatua migogoro ya taasisi hizo.

Ametoa kauli hiyo jana Julai 29, 2018 katika Kanisa la Pentekoste la Leganga, lililopo Arumeru mkoani Arusha.

“Kuanzia sasa, kanisa lolote au msikiti wowote utakaokumbwa na migogoro na kushindwa kuitatua wenyewe; misikiti hiyo, makanisa hayo nitakwenda kuyafuta mara moja,” alisema.

Alisema hatua hiyo inalenga kuhakikisha yanakuwapo makanisa na misikiti inayohubiri amani na utulivu.

Waziri Lugola ameonya askari Polisi wanaowashusha jukwaani masheikh na wachungaji inapofika saa 12:00 jioni, akisema muda huo ukifika waimarishe ulinzi ili waumini wamalize ibada zao vizuri.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: