Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akifanya uhakiki wa vipimo vya upana wa Daraja la Chipanga kama vinaendana na BOQ
Daraja la Chipanga lililo katika hatua za mwisho za umaliziaji wilayani Bahi
Viongozi wakikagua maabara iliyoanza kutoa huduma baada ya kumaliza kwa ujenzi katika kituo cha afya Bahi.
Zoezi la ukaguzi wa miradi likiendelea wilayani Bahi
Mbunge wa jimbo la Bahi Omary Baduel akiishukuru serikali kwa kufanikisha miradi ya maendeleo wilayani Bahi
Ujenzi wa daraja la Chipanga lililopo wilayani Bahi Mkoani Dodoma limeleta faraja kwa wananchi na viongozi wa wilaya hiyo huku wakimwagia sifa Wakala wa Barabara wa Mijini na Vijijini (TARURA) kwa usimamizi mzuri.
Hali hiyo imejidhihirisha leo katika ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo wilayani Bahi.
Akizungumzia kufurahishwa na ujenzi huo, Mbunge wa Jimbo la Bahi Omary Baduel amewapongeza TARURA kwa ujenzi wa daraja hilo kubwa na barabara zake kwa ubora wa hali ya juu ikilinganishwa na siku za nyuma kabla TARURA haijaanza.
Daraja la Chipanga ni daraja kubwa lenye urefu wa mita 45 na limegharimu Sh. bilioni 2.18 na litakuwa mkombozi kwa wananchi wa Chipanga ambao walikuwa wanateseka kwa miaka yote.
Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa pia kutembelea ujenzi wa kituo cha Afya Bahi kinacho karabatiwa na serikali kwa Sh.Milioni 500 ambapo hadi sasa kazi ya ujenzi imekamilika na wananchi wameanza kupata huduma katika majengo hayo yaliyojengwa kisasa.
Post A Comment: