Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo akimkabidhi vifaa vya michezo Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Gongoni Mwl. Mohamed Kikwayu.
Baadhi ya walimu wakuu wa sekondari wilayani Kisarawe pamoja na wanafunzi wa Minaki wakiwa katika zoezi la kupokea vifaa vya michezo kutoka kampuni ya Coca-Cola.
Walimu wa shule ya Msingi Kazimzumbwi wakiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo .
Wanafunzi wa Kazimzumbwi wakiwa katika picha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo amewataka wanafunzi kujenga upendo na kuacha ubinafsi katika kuipambania elimu.
Jafo ameyasema hayo leo katika ziara yake alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Minaki pamoja na walimu wakuu wote wa shule za sekondari zilizopo wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.
Amesema ni vyema wanapoipambania elimu wakawa na upendo na kuachana na ubinafsi. Katika ziara hiyo, waziri Jafo amefanikiwa kupokea vifaa vya michezo kutoka kampuni ya vinywaji ya Coca-Cola na kuwapatia wakuu wote 22 wa shule za sekondari zilizopo wilayani Kisarawe.
Pamoja na shughuli ya ugawaji wa vifaa vya michezo, Jafo ameungana na wananchi wa Kazimzumbwi katika zoezi la Kuboresha madarasa ya shule msingi ya kijiji hicho kwa kuchangia mifuko yote ya saruji ambayo itawezesha uwekaji wa sakafu katika madarasa yote na ofisi ya walimu ambayo hayajawekwa sakafu.
Zoezi hilo la uwekaji wa sakafu linatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi ili wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Kazimzumbwi wapate mazingira mazuri ya kusomea na kufundishia.
Post A Comment: