Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amewataka wakuu wa mashirika ya umma yaliyoshindwa kutoa gawiwo kwa Serikali kujitathimini kama wanastahili kuendelea kuyaongoza.

Dk Mpango amesema hayo leo Julai 10, 2018 jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongomano la kujadili jukumu la taasisi za umma katika utekelezaji wa sera ya viwanda lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi.

Akisoma hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyemtuma kumwakilisha, Dk Mpango alisema kuna jumla ya mashirika ya umma 270.

"Mimi katika nafasi ya waziri wa fedha na mipango, siridhiki na mashirika ambayo hayatoi gawio kwa Serikali," amesema Dk Mpango

“Wakuu wa mashirika husika na bodi wajitathimimi na nimekwisha muagiza Msajili wa Hazina, achambue na kufuatilia kwa karibu mienendo wa biashara na uongozi wa mashirika yote ili yale yasiyoenda vizuri tuondokane nayo lakini wahusika wawajibishwe,hatutaki kurudia makosa ya zamani," ameongeza

Amesema mashirika 232 yanamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100, mawili asilimia 50, manne zaidi ya asilimia 50 na mashirika madogo 32 kwa ubia ambayo nayo huenda yakabadilika kwa kuyaunganisha.

Dk Mpango amesema kati ya mashirika ya biashara 34 yanayomilikiwa kwa asilimia 100 na Serikali, mashirika 30 hayajatoa gawiwo ka mwaka 2016/17   .

Kati ya mashirika 36 yanayomilikiwa kwa ubia na wawekezaji,mashirika 20 hayajatoa gawio Serikalini.

Naye Msajili wa Hazina, Dk Athuman Mbuttuka amesema kongamano hilo ni muhimu katika kujadili namna ya kutekeleza sera ya viwanda.

Awali, Kadari Singo wa Taasisi ya Uongozi amesema kongamano hilo litajadili kwa kina adhima hiyo ya sera ya viwanda na jinsi inavyoweza kutekelezwa na kuchangia ukuaji wa maendeleo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: