Ofisa wa Uhamiaji Mkoa wa Kagera Abdallah Towo akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)juu y utendaji kazi wa uhamiaji Mkoa wa Kagera
Baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Ofisa wa uhamiaji Mkoa wa Kagera Abdallah Towo ofisini kwake
Na Editha Karlo ,Kagera.
JUMLA ya wahamiaji haramu 1470 kutoka mataifa mbalimbali wamekamatwa Mkoani Kagera kwa kuingia nchini kinyume cha sheria.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Ofisa uhamiaji Mkoa wa Kagera Abdallah Towo alisema kuwa kwa kipindi cha January hadi June 30 mwaka jumla ya wahamiaji haramu walikamatwa katika maeneo mbalimbali ya mipaka iliyopo Mkoani humo.
Towo alisema kuwa kati yao Warundi 994,Waganda 223,Warwanda 193,Wathiopia 19,wacongo 39 na wakenya 2 jumla yao ni 1470.
Alisema jumla ya raia 5,787 wa Burundi kutoka kambi za mtendeli,Nduta na Nyarugusu zilizopo Mkoani Kigoma pia kambi ya rumasi Ngara wamerejea nchini kwao kwa hiyari.Alisema jumla ya raia 90 kutoka Mataifa mbalimbali wamemaliza vifungo vyao katika Magereza yaliyopo mkoani Kagera na wote wamerejeshwa makwao.
"Kwa mwaka huu toka january hadi June hakuna mkimbizi yoyote aliyeingia nchini kwasababu kule kwao kwasasa kumetulia"alisema.
Ofisa Uhamiaji u huyo alisema kuwa zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya utaifa linaenda vizuri Mkoani Kagera na mpaka sasa jumla wananchi 491513 ili kupata vitambulisho vya utaifa lengo ni kuandikisha wananchi 1,200,000.
Alisema pia zoezi la uzinduzi wa hati za kusafiria za kielectronic kwa mkoa wa Kagera ulifanyika tarehe 8 mwezi wa 6 mwaka huu linaenda vizuri kwani mpaka sasa wameshapokea jumla ya maombi 72 na hati 64 zimeshatolewa na kukabidhiwa kwa wahusika.
Post A Comment: