Polisi nchini Uganda imefyetua gesi ya kutoa machozi na risasi hewani kutawanya kundi la waandamanji wanaopinga kodi iliyoidhinishwa ya kutumia mitandao ya kijamii.
Mwandishi wa BBC anasema polisi wamejaribu kumkamata mbunge ambaye pia ni muimbaji mashuhuri Robert Kyagulany, anayefahamika kwa umaarufu Bobi Wine, aliyeongoza maandamano hayo, lakini amefanikiwa kutoroka.
Mpiga picha mmoja katika maandamano hayo amekuwa akituma picha katika mtandao wa kijamii Twitter kuhusu yanayoendelea:
Bunge liliidhinisha kodi hiyo mnamo Mei baada ya rais Yoweri Museveni kushinikiza mageuzi hayo.
Rais Museveni a anaoutaja kuwa maoni, upendeleo, matusi na hata chati kwa marafiki.
Katika barua aliyomuandikia waziri wa fedha mnamo Machi, rais Museveni amesema kodi kwa mitandao ya kijamii inaweza kuongeza kipato cha serikali, na kupunguza mikopo inayochukua serikali na pesa za ufadhili.
Ameongeza kwamba haungi mkono kodi iitozwe kwa matumizi jumla ya mtandao kwasababu hili litaathiri matumizi yake kwa misingi ya 'elimu, na utafiti '.
Waziri wa habari na mawasiliano Uganda Frank Tumwebaze pia ametetea kuidhinishwa kwa kodi hiyo, akisema kwamba fedha zitakazopatikana zitatumiwa 'kuwekeza katika rasilmali zaidi za kimitandao'.
Inakadiriwa kwamba zaidi ya asilimia 70 ya raia nchini Uganda wana simu za mkononi.
Ni 41% ya raia nchini wanatumia mtandao Uganda kufikia mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter iliyo maarufu zaidi nchini humo.
Haya ni kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa wa mamlaka ya habari na taknolojia Uganda (NITA-U).
Mataifa mengine Afrika mashariki katika siku za hivi karibuni yamepitisha sheria za kudhibiti matumizi ya mitandao ambazo wakosoaji wanasema zinaathiri uhuru wa kujieleza.
Post A Comment: