Vyombo mbalimbali vya Habari nchini vimeguswa na kampeni ya usafi wa mazingira iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda na kuahidi kushirikiana kutoa elimu ya Usafi wa Mazingira kwa wananchi wa Dar es salaam.

Miongoni Mwa vyombo hivyo ni pamoja na ITV, TBC, Azam TV, Clouds TV, TV E, Star TV, Channel Ten na Radio Uhuru ambao wote kwa pamoja wamemuhakikishia RC Makonda kuwa watatumia media zao kujenga mtazamo chanya kwa wananchi juu ya umuhimu wa usafi wa mazingira.

Akizungumza kwenye kikao cha pamoja na watendaji wa Vyombo vya habari, Makonda amesema serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kutibu magonjwa yatokanayo na uchafu ikiwemo kipindupindu na malaria ndio maana ameona ni vyema kuanza kutoa elimu kwa wananchi ili kujua athari za uchafu kiafya badala kusubiri magonjwa yatokee ndipo wahangaike kutibu wagonjwa.

Aidha Makonda amesema anajisikia ufahari kuona vyombo vya habari vinashirikiana nae kwenye kampeni ya usafi wa Dar es salaam na kuwahimiza wananchi kuhakikisha wanaweka mazingira safi ilikuepusha kushurutishwa na vijana wa JKT na Mgambo watakaokuwa wakiwakamata na kuwatoza faini wachafuzi wa mazingira.

Kwa upande wao watendaji wa vyombo mbalimbali vya habari akiwemo Mkurugenzi mtendaji wa ITV Bi. Joyce Mhavile amesema watatumia vyombo vyao vya habari kutengeneza Vipindi na Makala za kuhimiza jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

Itakumbukwa kuwa Makonda ametangaza kuwatumia vijana waliohitimu Mafunzo ya JKT na Mgambo kufanya kazi ya kukamata na kuwatoza faini wachafuzi wa mazingira hivyo amona pia ni vyema Elimu ya umuhimu wa kutunza mazingira ikaenda sambamba.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: