Muda mfupi baada ya Tume ya Sayansi na Teknolojia, (Costech) kusema wamesikitishwa na kitendo cha kusambaa mitandaoni kwa barua waliyowaandikia taasisi ya Twaweza, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Aidan Eyakuze amesema hawajahusika kuisambaza.

Eyakuze ameyasema hayo leo Julai 12, kwenye ukurasa wa twitter wa taasisi hiyo.

“Kama tulivyosema awali, tumepokea barua kutoka Costech na tunaifanyia kazi. Twaweza haijasambaza barua hiyo wala kuhusika kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii,” imesema taarifa hiyo

Eyakuze amesema, barua zote zinazopelekwa Twaweza huwekwa muhuri mbele ya aliyetumwa kuipeleka pamoja na risiti.

“Barua inayosambaa mitandaoni haina muhuri wetu, tunaheshimu mawasiliano yote yanayofanywa na wadau wetu,”amesema

Leo Kaimu Mkurugenzi wa Costech  Dk Amos Nungu alizungumza na wanahabari na kusema wamesikitishwa na kusambaa mitandaoni  kwa barua hiyo waliyopelekewa Twaweza

Share To:

msumbanews

Post A Comment: