Na, magdalena kashindye.
Waziri wa kilimo Charles Tizeba amewataka wakulima wa tumbaku wilayani Kahama mkoani Shinyanga kuachana na kilimo cha kutegemea Mkopo kwakua kinazoofisha soko la zao hilo

Tizeba ametoa wito huo wakati akiwahutubia wakulima wa halmashauri ya ushetu iliyopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga katika uzinduzi wa bima ya Afya kwa wakulima iliyoziduliwa na waziri Mkuu Kasim Majaliwa.

Tizeba amesema soko la tumbaku limekua likizoofu kila siku kutokana na wakulima kuingia kwenye madeni na kampuni moja ambalo hulazimika kuwauzia  pindi wanapovuna na hali hiyo haileti ushindani wa soko.

Aidha tizeba amewataka wakulima kuanza kutunza akiba mwaka huu ili msimu ujao wa kilimo wasikope tena na waweze kuuza zao hilo kwa njia ya mnada.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: