Uongozi wa Azam Media kupitia Mkurugenzi wake, Tido Mhando, umeibuka na kukanusha taarifa zilizoelezwa kuwa hawatoonesha mechi za Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Mhando amefunguka na kueleza kuwa taarifa zilizosambaa katika mitandao mbalimbali zikieleza kuwa Azam haitorusha mbashara mechi za ligi msimu wa 2018/19 si za kweli.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa Azam bado wana misimu mitatu hivyo mkataba wao utakapomalizika watakuwa tayari kufanya mazungumzo mengine ya kuongeza lakini si kweli kuhusiana na yaliyoripotiwa jana.
Ikumbukwe Azam Media waliingia mkataba na TFF kupitia klabu zote za ligi na kusaini mkataba wa kurusha mechi za ligi mpaka msimu wa 2020/21 ambapo mkataba huo utakuwa unamalizika.
"Si kweli kwamba tutasitisha kuonesha, hizo habari hazina ukweli wowote, tutaendelea kama kawaida na mkataba wetu unaoenesha bado tuna misimu mitatu ya kuendelea kuonesha mechi hizo" alisema.
Post A Comment: