Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula kupitia radio Kwa Neema FM amesema Serikali ya CCM chini ya uongozi wa awamu ya tano wa Mhe Dkt John Pombe Magufuli imeboresha huduma ya Afya Nyamagana.
Katika mwaka huu wa fedha 2018-2019 imepandisha hadhi Zahanati ya Igoma kwa kuwa kituo cha Afya rasmi kwa kutoa shillingi 400,000,000 kwa ajiri ya ujenzi wa Vyumba saba ikiwemo, Chumba cha Upasuaji, chumba cha kujifungulia, wodi ya Mama na Mtoto, Mapokezi, chumba cha usafi pamoja na chumba cha kuhifadhia marehemu.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Post A Comment: