Mkuu Wa Nchi wa Shirika la Compassion Nchini, Agnes's Hotay akizungumza katika Mahafali ya Nne ya kuondoka kwenye ufadhili Wa shirika hilo kwa watoto waliokuwa wakilelewa kwenye Klasta ya USA River, wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha .
Wahitimu
Na Pamela Mollel,Arusha
Serikali imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuanza kuwekeza kwa watoto hasa wanaoishi katika mazingira Magumu ili kuepusha dhana ya kuwa na taifa lenye watoto ombaomba.
Kauli hiyo aliitoa Mkuu Wa Nchi wa Shirika la Compassion Nchini, Agnes's Hotay alipokuwa kwenye Mahafali ya Nne ya kuondoka kwenye ufadhili Wa shirika hilo kwa watoto waliokuwa wakilelewa kwenye Klasta ya USA River, wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha baada ya kufikisha umri Wa Miaka 22 .
Hotay amesema kuwa ipo haja kwa serikali kuunga mkono jitihada zinazoonyeshwa na Mashirika , taasisi mbalimbali katika kuwahudumia watoto waliopo katika mazingira magumu kwa kuwapatia elimu na ujuzi ili waweze kujiajiri ,jambo litakalosaidia kupunguza namba ya vijana wasio na ajira .
Amesema shirika hilo hapa nchini limeifikia mikoa 17 na linafanya kazi na makanisa wenza zaidi ya 400 na linahudumia watoto zaidi ya 93,000 ikiwa lengo ni kuwaondoa watoto kwenye umasikini na kuwajengea uwezo Wa kujitegemea,kujikinga na maradhi na kuwajenga kiuchumi.
Alitoa rai kwa wahitimu kuhakikisha wanakuwa waadilifu kwa kuzingatia yale mema yote waliofundishwa na walimu wao.Awali katika risala ya wahitimu hao wapatao 78 walilishukuru shirika la Compassion kwa ufadhili huo ambao umewasaidia kuwajenga kiroho,kuwapatia Elimu ya ujasiliamali na kutaka makanisa mengine kuinga mfano huo utakao saidia kupunguza changamito za vijana.
Naye Mwenyekiti wa Klasta ya USA River ,Saluni Kisangas amesema Shirika hilo kwa kushirikiana na Makanisa wenza limekuwa likiwahudumia watoto tangia wakiwa na umri mdogo wa kuingia chekechea na punde wanapofikisha umri wa miaka 22 wanaamini umri huo wanastahili kujitegemea.
Aidha amesema katika Klasta ya USA River inayohudumia kata 4 ,tangia kuanzishwa kwa Klasta hiyo mwaka 1999 ambapo wahitimu wengi wamenufaika na Mpango huo kwa kupata ajira serikalini na baadhi yao kuchukuliwa na mashirika Mbalimbali.
Post A Comment: