Waziri wa elimu, sayansi,teknolojia na mafunzo ya ufundi Profesa Joyce Ndalichako ,amesema serikali imeweka mkakati wa ujenzi wa shule mpya za kidato cha tano na sita pamoja na kuboresha miundombinu katika shule zilizopo ili kukidhi idadi kubwa ya wanafunzi wanaofaulu vizuri na kukosa nafasi hasa baada ya zaidi ya wanafunzi elfu 21 kukosa nafasi mwaka huu katika shule za serikali.
Waziri Ndalichako ameyasema hayo wilayani Kasulu mkoani Kigoma baada ya kukutana na wadau wa elimu na kuzindua albam ya kwaya katika kanisa la pentekoste FPCT ambapo ameeleza mkakati huo wa serikali na kuwa wanafunzi wengine waliofanya vizuri watapelekwa kwenye vyuo vya kati na wengine watakwenda shule binafsi na kwamba serikali haitatoa ada elekezi kwa shule binafsi bali itashirikiana na wadau kuhakikisha elimu inayotolewa ni bora.
Kwa upande wake kaimu askofu wa kanisa la Pentekoste FPCT Kasulu Shadrack Bunolo ameitaka serikali kuongeza ushirikiano na shule binafsi nchini ili elimu inayotolewa kwa watoto iwe bora na yenye manufaa kwa jamii.
Post A Comment: