Na said Mwishehe,

SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeamua kuwanoa viongozi wanawake wa ngazi mbalimbali wakiwamo madiwani na wakuu wa Idara katika manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu maadili ya viongozi wa umma. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati anafungua semina ya mafunzo hayo Kamishina wa Sekratarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Harold Nsekela amesema yatatoa fursa kwa viongozi hao kufahamu sekretarieti kuanzia majukumu, kazi na wajibu walionao katika usimamizi wa maadili.

Amefafanua sababu za kutolewa kwa mafunzo yametokana na utafiti uliofanywa mwaka 2015 kupitia taaaisi yao ya Kukuza uelewa wa wananchi kuhusu majukumu na kazi zinazotekelezwa na sekretarieti hiyo. "katika utafiti huo iliyokuwa unapoona ushiriki wa utoaji wa taarifa uliofanywa na makundi mbalimbali katika jamii kuhusu ukiukwaji wa maadili miongoni mwa viongozi wa umma. 

"Matokeo yalionesha ni asilimia moja tu ya wanawake kwenye vijiji na mitaa walishiriki kutoa taarifa za ukiukwaji wa maadili, "amesema. 

Amesema hali hiyo ililazimu Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kuandaa mafunzo hayo katika mikoa yote inayotekelezwa mradi huo ambayo ni Mtwara, Morogoro, Iringa na Dodoma. "Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uelewa viongozi wanawake katika mamlaka za Serikali za mitaa kuhusu maadili ya viongozi wa umma.

"Baada ya kupata mafunzo haya nanyi muweze kuwahamasisha na kuwaelimisha wanawake wengine katika ngazi za chini kwenye mitaa na Kata kwani tunaamini hiyo itanisaidia kuwajengea ujasiri wa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika pindi wanapokumbana na ukiukwaji wa maadili, "amesema.Ameongeza ikumbukwe moja ya misingi ya demokrasia ni kuwa na Serikali inayowajibika kwa wananchi na yenye viongozi wanaotumikia wananchi kwa uadilifu.

"Wananchi wanategemea viongozi wanatumia nafasi zao za uongozi kuwaletea maendeleo na si vinginevyo.Tunafahamu uongozi ni dhamana. Kiongozi yoyote awe wa kuchaguliwa au kuteuliwa amekabidhiwa madaraka na wananchi,"amesema.

Pia amesema uadilifu ni sharti ujengwe ndani ya jamii ili uwe sehemu ya utamaduni wa nchi na kufafanua sheria ya maadili ya viongozi wa umma, kanuni za Serikali za mitaa pamoja na vyombo vya kusimamia utawala bora pekee haviwezi kufanikisha bali ni jukumu la kila mmoja wetu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: