Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexender Pastory Mnyeti amewanyooshea kidole wapinzani kwa kuwaeleza kuwa katika mkoa wake hataki kusikia siasa uchwara.
Akiwa katika ziara yake ya kawaida akisikiliza kero za wananchi katika mji wa Babati alianza kwa kueleza kuwa anamshangaa mbunge wa Babati mjini Paulina Gekul [CHADEMA] kuwaeleza wananchi kuwa mbaazi imekosa bei wakati bungeni wanatoka nje wakati wa vikao na kuongeza kuwa hata bajeti waliipinga.
“Nimemsikia mbunge wenu anazungumzia bei ya mbaazi,niseme hapa sio sehemu ya siasa,mambo ya mbaazi angezungumza bungeni sio katika mkutano,mimi ndiyo mwenye mkutano, ninachowaomba ndugu zangu wa Babati achaneni na siasa uchwara endeleeni kufanya maendeleo yenu, kwa sasa ilani inayotekelezwa ni ya Ccm ,” alisema Mnyeti.
Ameendelea kwa kusema kuwa hataki kuona mikutano ya kisiasa katika mkoa wake isiyo kuwa na maana na kueleza kuwa akiona mikusanyiko yeye mwenyewe ataisambaratisha.
Rc Mnyeti alikuwa na ziara ya kikazi ya siku 5 katika mji wa Babati akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na wilaya pamona na wakuu wa idara mbalimbali na kote alipotembelea alisikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Post A Comment: