Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amejifungua mtoto wa kiume kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa kupitia mtandao wa Instagram.
Mapema leo mkuu huyo alipost picha ya video mtandaoni na kuandika taarifa hiyo ya kupata mtoto wake ambaye ampatia jina la Keagan.
“Mungu wewe ni waajabu tena unatenda Kwa wakati wako. Asante Kwa ZAWADI YA MTOTO WA KIUME @ KEAGAN P MAKONDA,” aliandika RC Makonda kupitia instagram.
Faraja Nyalandu amempongeza mkuu huyo kwa kuandika, “Maria na Paul, nilishuhudia mkiapa kiapo cha ndoa takatifu na leo nashuhudia mkiwa baba na mama Keagan. Hakika Mungu wetu ni mwaminifu, njia zake sio kama zetu. Kama mbingu zilivyo juu ndivyo mipango Yake ilivyo juu ya waaminio @paulmakonda
Post A Comment: