RAIS Dk.John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kitaifa wa tamasha la maalum la Mwezi wa Urithi kuenzi utamaduni wa Mtanzania ambalo litafanyika nchini nzima kwa kuaza na Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangala amesema Serikali kupitia wizara hiyo wameaandaa tamasha hilo ambalo linalenga kuenzi utamaduni na urithi wa Mtanzania na kwamba tamasha hilo linaitwa Urithi Festival ambalo litakuwa likifanyika kila fikapo Septemba ya kila mwaka kuanzia mwaka huu.

"Dhumuni la tamasha ni kuenzi na kunadi kiutalii hazina kubwa ya utamaduni ,mila na desturi za makabila yote nchini ambayo ni zaidi ya 128.Hatua hii inaenda sambasamba na juhudi za Serikali za kuongeza wigo wa mazao ya utalii nchini hususan kukuza matumizi endelevu ya malikale,kutangaza utamaduni , vyakula vya asili , michezo ya jadi na kazi za sanaa mbalimbali.

"Tamasha litaisaida pia kukuza utalii wa ndani na kuongeza wastani wa watalii wa kimataifa kukaa nchini , hatua itakayoleta matokeo chanya kwenye mapato yatokanayo na sekta ya utalii na malikale.Wadau wa mwezi wa Urithi wa Tanzania ni Watanzania wote chini na waliopo ughaibuni .

"Aidha tamasha linawalenga raia wa mataifa mengine wanaoishi Tanzania na watalii wa kimataifa na kwamba tamasha litawashirikisha wadau wote wa utalii,"amesema Dk.Kigwangala.

Kuhusu namna ya kushiriki Dk.Kingwangala amesema Urithi Festival itasheherekewa Septemba yote na kwamba tamasha litafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri ambapo patakuwepo na matukio mbalimbali yakiwamo maonesho ya ubunifu wa sanaa na tamaduni , kazi za wajasiriamali na wadau wa utalii.

Ameongeza ambapo pia kutakuwa na maonesho ya vyakula na vinywaji pamoja a burudani za ngoma kutoka katika makabila ya mkoa wa Dodoma na mikoa jirani , muziki wa dansi na kizazi kipya.Pia watatemdelea michoro ya Miambani ya urithi wa dunia ya Kondoa .

"Septemba 8 mwaka huu patakuwa na uzinduzi wa kitaifa wa Urithi Festival katika uwanja wa Nyerere Square Dodoma.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dk.Magufuli.Wiki ya kilele inatarajiwa kufanyika mkoani Arusha kuanzia Septemba 24 mpaka 29 mwaka huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo nako kutakuwa na matukio mbalimbali.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,"amesema.

Ameongeza pamoja na kufanyika Dodoma na Arusha pia tamasha la Urithi Festival litafanyika nchi nzima kwa mwaka huu ambapo Wizara itaanza na Majiji ya Dar es Salaam ,Mwanza na Mji Mkongwe-Zanzibar(Septemba 10 mpaka Septemba 16) na Mwanza (Septemba 17 mpaka 23).Dk.Kigwangala ametumia nafasi hiyo kuelezea kuwa kuna kila sababu ya Watanzania kushiriki kwenye tamasha hilo na kwa walio nje ya nchi ni vema nao wakaja kuona namna ambavyo shughuli za kiutamaduni na malikale zinavyoenziwa.

Ametoa rai kwa Watanzania pia kujenda utamaduni wa kutemebela vivuto vya utalii na hifadhi mbalimbali zilizopo nchini na kufafanua gharama ziko chini , hivyo kila mtu anaweza kwenda.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: