Rais Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika nafasi mbalimbali za kiungozi kama ifuatavyo;
Rais John Magufuli amemteua Jokate Mwegelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani
Rais pia amemteua Jerry Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha.
Patrobas Katambi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.
Wakati huo huo, David Kafulila ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.
Moses Machali ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara
Lengay Ole Sabaya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro
Daniel Godfrey Chongolo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar Es Salaam.
Rais Magufuli amemteua Ally Hapi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa , kabla ya uteuzi huo Hapi alikuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni.
Dr Jim Yonaz ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano
Post A Comment: