Clerance Kipobota kutoka Shirika la Freedom House ambaye amemwakilisha mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo akifungua semina ya (Alternative Media) kwa waandishi wa habari za Mitandao ya kijamii (Online Platform Reporters) inayofanyika kwenye Hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
.....................................................................
Shirika la Kimataifa la Freedom House linaendesha mafunzo kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii 'bloggers' kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu namna kuendesha vyombo vya habari mbadala.
Mafunzo hayo ya siku mbili ‘Julai 26 – 27,2018’ kuhusu Vyombo vya habari mbadala ‘Alternative Media’ yaliyoratibiwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) yanafanyika katika ukumbi wa Flomi Hotel mkoani Morogoro.
Awali akifungua mafunzo hayo,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa shirika la Freedom House Clarence Kipobota alisema kupitia mafunzo hayo waendeshaji wa mitandao ya kijamii watajifunza mbinu mbalimbali kuhusu namna ya kuendesha mitandao yao.
“Tutajengeana uwezo na kujadili na kuunda jukwaa moja la waandishi ambao wanatumia Alternative Media”,alieleza.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mwezeshaji wa semina hiyo Bw. Daniel Lema akitoa mada kwa waandishi wa habari katika semina inayofanyika katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Mwezeshaji John Kaoneka akitoa mada katika semina hiyo kuhusu mitandao ya kijamii.
Afisa Mafunzo , Utafiti na Machapisho UTPC Victor Maleko akiwa katika semina hiyo.
Picha mbalimbali zikionyesha washiriki wa semina hiyo
Waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua semina hiyo.
Post A Comment: