Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema hawezi kukihama chama hicho tawala kwa kuwa ana hisa nyingi.

Nape ametoa kauli hiyo jana jioni Jumapili Julai 15, 2018 mbele ya  wananchi wa Mtama ambao jioni hiyo alijumuika nao kutazama fainali za kombe la Dunia..

Amewataka wananchi hao kuondoa hofu juu yake akiwataka kupuuza maneno yanayosemwa kuhusu hatima yake CCM ambapo alisisitiza kuwa hataondoka katika chama hicho.
Kuhusu asilimia 65 ya ushuru wa zao la korosho kwenda Serikali Kuu, Nape amesema ataendelea kufuatilia jambo hilo na kusisitiza kuwa kuteleza si kuanguka.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: