MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo amepokea mwenge wa uhuru ,ukitokea jijini Dar es salaam ,ambapo ukiwa mkoani hapo unatarajiwa kupitia miradi ya maendeleo 67 yenye thamani ya sh.bilioni 162.440.8 .
Kati ya miradi hiyo ,16 itawekwa mawe ya msingi ,miradi 13 itazinduliwa ,nane itafunguliwa na 21 itakaguliwa.Akikabidhiwa mwenge huo ,wilayani Mkuranga Ndikilo alisema ,mwenge wa uhuru ukiwa mkoani humo, pia utapitia wilaya 7 na halmashauri 9#.
Alisema mwenge wa uhuru utapokea taarifa ya miradi 9 katika maeneo mbalimbali ya mkoa na wamehakikisha miradi yote itakuwa na thamani ya fedha ili wasiangukie kwenye mtego ambao uliwakumba mkoa wa Dar es salaam.
Alieleza ,miradi hiyo imetekelezwa kwa ushirikiano baina ya wananchi,serikali kuu,halmashauri na wahisani wa kitaifa na kimataifa." Kaulimbiu ya mbio za mwenge kwa mwaka huu ni ‘Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’
"Katika kutekeleza ujumbe huo tumejipanga kutekeleza kwa vitendo ambapo kwenye elimu tumevuka lengo kwa kuandikisha watoto wa darasa la kwanza." alisema Ndikilo.Mkuu huyo wa mkoa alieleza ,mwaka huu lengo ilikuwa 47,686 walioandikishwa ni 52,551 sawa na asilimia 110.
Ndikilo alisema ,katika upande wa viwanda wamefanya kazi nzuri kwani kwasasa wana viwanda zaidi ya 400 vikubwa ,vya kati na vidogo."Asilimia 20 ya ajira zote viwandani Pwani ni za wazawa wa mkoa na wanatarajia kufikia asilimia 50." alielezea Ndikilo.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu Charles Kabeho, alihimiza elimu kwa watoto wote na kuwataka wazazi kuwa na mwamko wa kuwapeleka watoto shule.Mwenge huo umeanza mbio zake July 12 wilayani Mkuranga Mkoani Pwani na July 13 unatarajiwa kupokelewa wilayani Rufiji.
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo akimpokea kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu ,Charles Kabeho ,wilayani Mkuranga mkoani hapo.(picha na Mwamvua Mwinyi).
Post A Comment: