MSEMAJI Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abbasi ameelezea kinachoendelea katika utekelezaji wa ahadi za Serikali huku 
akitumia nafasi hiyo kuwasisitiza wanahabari wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa maadili ya kiwango cha juu.

Akizungumza na waandishi mbalimbali Mjini Dodoma Dk.Abbasi ameanza kwa kuwapongeza waandishi wa habari kwa ushirikiano ambao wamekuwa wamekuwa wakiutoa katika kusaidia mwaka wa fedha 2017/2018 katika kusaidia kuhabarisha umma masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za Serikali.

Hata hivyo amesema bado wamendelea kushuhudia kuwepo kwa vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya taaluma kwani pale Serikali itakapochokua hatua kusiwe na lawama.Pamoja na hayo akafafanua mambo mbalimbali nchini ambapo katika hali ya uchumi Dk.Abbasi amesema hadi Machi mwaka 2017 pato la Taifa lilikuwa kwa wastani wa asilimia 7.1 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.0 kwa mwaka 2016.

Amesema ukuaji huo ulitokana na na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na kuimarika kwa shughuli za kiuchimi."Kilimo kutoka asilimia 2.1 hadi asilimia 3.6, mawasiliano kutoka asilimia 13.0 hadi asilimia 14.7, madini kutoka asilimia 11.5 hadi asilimia 17.7 na ujenzi kutoka asilimia 13.0 hadi asilimia 14.1,"amesema Dk.Abbasi.

Pia amesema maji kutoka asilimia 4.3 hadi asilimia 16.7 , uchukuzi kutoka asilimia 11.8 hadi asilimia 16.6, elimu kutoka asilimia 8.1 hadi asilimia 8.5 na afya kutoka asilimia 5.2 hadi asilimia 5.9.Kwa taarifa zaidi kuhusu ambacho Dk.Abbasi amekielezea kwa watanzania kupitia waandishi wa habari na kufafanua kwa kina kupitia maelezo yake ambayo yamewekwa kama yalivyo

HAPA CHINI


Share To:

msumbanews

Post A Comment: