Kiungo  na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Croatia, Luka Modric ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na kupewa Mpira wa Dhahabuwakati timu yake ikipoteza mchezo wao wa fainali kwa kukubali kichapo cha bao 4-2 kutoka kwa Ufaransa huko Urusi.

Modric ambaye amemaliza mashindano akiwa na mabao mawili, ameisaidia timu yake kutinga fainali ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kufikia hatua hiyio kubwa ya kihistoria.

Modric amewashukuru mashabiki wa Croatia na wachezaji wenzake kwa sapoti kubwa waliowapa hadi kufikia fainali licha ya kufungwa.

Mbelgiji, Eden Hazard amekuwa mchezaji Bora wa Pili na kutunukiwa mpira wa Silver, na Mfaransa, Antoine Griezmann ameibuka mchezaji Bora wa Tatu na kupewa mpira wa shaba.

Wachezaji wengine ambao wamewahi kubeba tuzo hiyo ni pamoja na Lionel Messi, Zinedine Zidane, Ronaldo de Lima, Davor Suker, Diego Maradona na Paolo Rossi. 

Tuzo hii, inamuweka Modric katika nafasi nzuri ya kushinda tuzo ya mwaka huu ya Ballon d'Or.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: