Na John Walter Babati
Mkuu wa mkoa wa MANYARA Alexender Pastory Mnyeti ameiagiza idara ya ardhi mjini Babati kutoa hati miliki kwa wote wenye viwanja Maisaka A Babati Mjini ndani ya siku tisini.
Agizo hilo amelitoa kwenye mkutano wa wananchi uliofanyika Julai 25 katika shule ya msingi Sinai kusikiliza malalamiko ya wakazi wa Maisaka.
Kwa mujibu wa Mnyeti,agizo hilo ni la Rais Magufuli baada ya kusoma na kutazama taarifa ya Habari baada ya nyumba zilizokuwa zimejengwa kiholela katika eneo la Maisaka A kuwekewa alama ya X iliyosababishwa na uzembe wa idara ya ardhi na mipango miji.
Mnyeti amesema kuwa hati hizo atakabidhi mwenyewe kwa wananchi tarehe 25 Oktoba mwaka huu na kuwataka wananchi wote ambao bado nyumba zao zina X wakazifute waishi kwa uhuru.
"Kwa Tanzania ukitaka kubomoa waliojenga Kiholela ni asilima 75% serikali imeona iwaache ambao tayari wameshajenga kwa sababu serikali kupitia idara ya Ardhi na Mipango miji ilishakosea kuwaachia watu hao kujenga bila kufuata utaratibu” alisema Mnyeti.
Hata hivyo ametoa onyo kwa wanaoendelea kujenga katika maeneo ambayo sio rasmi huku akitoa onyo kwa waliojenga kwenye milima.
Post A Comment: