Mkuu wa Wilaya ya Same,Rosemary Staki Senyamule akipokea Mbuzi kwa mmoja wa wananchi ikiwa ni sehemu ya kuchangia ujenzi wa madarasa 50 yaliyokusudiwa kukamilia ifikapo Novemba, 2018 mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Same,Rosemary Staki Senyamule akipokea vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ua Saruji na Mabati kutoka Wananchi ikiwa ni sehemu ya kuchangia ujenzi wa madarasa 50 yaliyokusudiwa kukamilia ifikapo Novemba, 2018 mwaka huu.
Baadhi ya Wanafunzi wakiwa wamekaa nje ya jengo la shule ambalo linatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
WADAU mbalimbali wilayani Same wamekumbushwa kukamilisha ahadi zao ili kufanikisha ujenzi wa madarasa 50 yaliyokusudiwa ili ifikapo Novemba, 2018 mwaka huu yawe yamekamilika.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Same,Rosemary Staki Senyamule wakati akizungumzia michango ya ujenzi wa madarasa hayo ambapo kata 10 ambazo zimekamilisha michango zimekabidhiwa fedha za kukamilisha majengo.
Uzinduzi umefanyika katika Shule ya Msingi Moipo iliyopo katika Kata ya Mabilioni.Hivyo moja ya mambo ambayo wadau wamekumbushwa ni kukamilisha ahadi ili kazi hiyo ikamilike.Uzinduzi wa ujenzi umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Mkuu wa Wikaya ya Same, Mwenyekiti wa Halmashauri, Diwani na wataalamu.
" Ukamilishaji wa madarasa haya utawezesha watoto 2250 kupata madarasa ya uhakika ya kusoea,"amesema Mkuu wa Wilaya hiyo wakati anawashukuru wananchi waliochangia.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ameahidi kusimamia vizuri michango hiyo na kuagiza kuwe kunatolewa taarifa ya matumizi kwa wananchi.
Wakati huo huo wananchi wahimizwa kuhakikisha watoto wanaenda shuleni ili kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli na Serikali yake ya kutaka watoto wote wapate elimu bure, wale watoro wazazi wao kushughulikiwa.
" Elimu bora ni wajibu wa kila mwanajamii".
Post A Comment: