Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo , John Kayombo ambaye pia ndio Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri hiyo akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo kuwa Ndugu Pascal Manota kapita bila kupingwa.
Diwani Mteule wa Chama Cha Mapinduzi Pascal Manota akipokea barua ya kuwa Mshindi wa uchaguzi mdogo kwa kupita bila kupingwa mara baada ya kuwashinda wapinzani wake kwa mapingamizi
Diwani Mteule wa Chama Cha Mapinduzi Pascal Manota akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kutangazwa mshindi
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam John Kayombo amemtangaza Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Pascal Manota kuwa mshindi katika uchaguzi mdogo ulioitishwa nchini katika Kata ya Kimara.
Kayombo amemtangaza Manota kuwa Diwani Mteule kutokana na madiwani wengine kutoka vyama upinzani kushindwa kujibu hoja za mapingamizi aliyowawekea kama mapungufu wakati wa ujazaji wa fomu.
“Vyama vilivyoweza kuchukua fomu ya kugombea Udiwani katika Kata ya Kimara ni , ACT-Wazalendo, Chadema, CUF na CCM lakini kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika ujazaji wa fomu Pascal Manota namtangaza kama Diwani Mteule aliyepita bila ya kupingwa,”amesema Kayombo.
Kwa Upande wake Manota ambaye ni Diwani Mteule katika Kata ya Kimara amewetaka wapinzani kuacha siasa za uongo za kuwasingizia watendaji kuwa ndio wanaharibu uchaguzi wakati wao ndio wa kwanza kuvunja taratibu za uchaguzi na sharia zilizowekwa.
Amesema wagombea wote walichukua fomu na zikajazwa na kubandikwa katika mbao ya matangazo katika Kata, hivyo baada ya kuona mapungufu ya wagombea wake aliamua kuwawekea mapingamizi.Kutokana na mapingamizi hayo wagombea wote wametupwa nje.
Amesema kuwa sasa anasubiri kuapishwa ili aendelee kuwatumikia wakazi wa Kimara na hatimaye wapate maendeleo ya kweli kupitia Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli.
Post A Comment: