Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini (CUF), Selemani Bungara maarufu kama 'Bwege' amefunguka na kudai katika viongozi ambao anawapenda katika nchi hii ni Rais Dkt. John Magufuli huku akimuomba asimamie haki za wananchi kwani akifanya hivyo ataweza kushinda hata miaka 100.
Bwege ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kwenye ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana hadi saa 10 alasiri na kusema hilo ndio jambo kubwa ambalo alitaka kulisema ili kusudi liweze kumfikia Rais Magufuli kwa kuwa ameweza kurejesha heshima katika baadhi ya maeneo ambayo hapo awali yalikuwa ya hovyo.
"Katika kiongozi ambaye mimi nina mpenda ni Rais Magufuli maana ameweza kurejesha nidhamu katika ofisi za Utumishi wa Umma. Hilo amefanikiwa sana lakini bado naendelea kumuomba sana asimamie utawala wa sheria. Watanzania wote wanamuamini Dkt. Magufuli yeye ni kichwa", amesema Bwege.
Pamoja na hayo, Bwege ameendelea kwa kusema "akifanya hivyo tu ataendelea kushinda hata miaka 100, lakini yote mazuri ambayo ameyafanya kama hatosimamia haki za wananchi hali haitokuwa nzuri".
Post A Comment: