Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula amewaambia wadau wa Filamu amedhamiri kuinua tasnia ya Filamu ili iwe ajira sanjari na kuchangia pato la taifa.
Mhe Mabula amebanisha hayo alipokutana na wadau wa Filamu chini ya Afisa Utamaduni Jiji la Mwanza. Wakiwa ni Chama Cha wasambazaji wa Filamu UBIFIMU, Chama Cha waandaaji Filamu CHAWAFITA pamoja na Chama Cha waigizaji wa Filamu. Mhe Mabula amewapongeza Wadau hao kwa kupokea ushauri wake kujiunga katika vikundi ili iwe vyepesi kuweza kunufaika na 10% ya fedha ya halmashauri ya Jiji la Mwanza tengo la 5% kwa Vijana na 5% kwa wanawake.
Mhe Mabula amepokea mapendekezo ya kuzungumza na serikali kuweka ofisi ndogo ya BASATA pamoja na COSOTA ili kurahisisha huduma ya usajiri. Pamoja na kuzungumza na TRA tawi la Mwanza kuweka utaratibu wa kutoa Stika za kazi ya wasanii kuliko kuzifuata huduma hizo Dar Es Salaam.
Ambapo wadau hao wamemwambia Mhe Mbunge, imekuwa ikiwagharimu raslimali muda na fedha kusafiri kwenda Dar Es Salaam ili kupata huduma ya stika kwaajili ya kazi ili waweze kuzisambaza sokoni. Kadharika kufuata huduma za usajili COSOTA na BASATA Dar Es Salaam.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Post A Comment: