Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula ameendelea na ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kata ya Kishiri, ambapo amepata fursa ya kutembelea Zahanati ya Fumagila Kukagua miundombinu, huduma pia kupokea changamoto.

Mhe Mabula akiwa Zahanati ya Fumagila ameuomba uongozi wa Zahati hiyo kuwahudumia wananchi kwa moyo wa utayari na uzalendo maana serikali imejitahidi kusogeza huduma kwa jamii sanjali na kuongeza bajeti ya fedha za Vifaa Tiba na Madawa kwa wakati na kwa 96%-98% Wilayani Nyamagana. Mhe Mabula amepokea ombi la Mganga mkuu aliyeomba Mhe Mbunge kupitia ofisi yake kwa ushirikiano wa wadau wa maendeleo wawezeshe kusaidia ununuzi wa Kitanda cha kujifungulia wa Mama wajawazito.

Akifafunua Changamoto zinazokabiri Zahanati hiyo Mganga Mkuu alitumia fursa hiyo kumshukuru Mhe Mabula kwa Msaada wa Umeme wa Jua walioupokea  kutoka kwake wenye uwezo wa 80 Watt na kulingana na mahitaji wameomba pia wawezeshe Umeme wa Jua wenye uwezo wa  200 watts. Kisha akamalizia na Ombi la kupata kampuni ya ulinzi utakao wezesha  Ulinzi wa uhakika eneo hilo kwa masaa 24.

Mhe Mabula amehitimisha ziara yake kwa kumjulia hali Mwenyekiti wa Mtaa wa Kaniwa ambaye anaumwa kwa muda mrefu Kiharusi.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: