Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula mapema leo ametembelea ofisi za kanda za Shirika la Utangazaji Tanzania lenye ofisi zake   Capripoint kata ya Nyamagana wilaya ya Nyamagana.

Mhe Mabula akiwa ofisini hapo amepata fursa ya kuzungumza na meneja Kanda Bi Rachel Macha kuwa amelenga kuvifikia vyombo vyote vya habari vilivopo Nyamagana sanjari na taasi zote zenye makao yake makuu Nyamagana. Mhe Mabula amepongeza taasi hiyo ambayo ipo imara kutoa habari za jamii kwa uharaka kupitia vipindi Mbashara, taarifa za habari, vipindi maalumu vya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi  wa Chama Cha Mapinduzi 2015-2020. Mie ni mpenzi wa kipindi tunatekeleza, pamoja na kipindi cha Jimbo langu" Mhe Mabula alisema.

Maneja kanda TBC kanda ya Ziwa Bi Rachel amesema shirika la  utangazaji linafanya kazi katika mikoa Sita Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera. Ina wafanya kazi 25 na lengo kuu miaka ya baadae ni kuwa na waandishi wake kila wilaya ili kuongeza ufanisi wa uharaka wa upatikanaji wa habari. Bi Rachel amempongeza Mhe Mabula kuwa mbunge wa mfano kuzitembelea ofisi hizo. Amewaasa wawakilishi wa wananchi kutumia TBC taifa na TBC1 kuelezea utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kadharika amemuomba Mhe Mabula kupitia nafasi yake kuweka meza ya mazungumzo na familia nne zilizovamia eneo la mnara wa TBC  na kujenga. Naye Mhe Mabula amemhaidi kuita afisa ardhi katika halmashauri ya Jiji la Mwanza kupitia ramani ya eneo hilo kisha kuona waanzie wapi.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: