Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus ameendelea na ziara  Kata mbili, ikiwa ni kata ya Igogo pamoja na Mbugani kukagua Mradi mkubwa wa maendeleo wa mfumo wa majitaka unaowezesha ujenzi wa vyoo 295 pamoja na barabara kufikia maeneo ya miinuko. Utekelezaji wake umetumia miezi 15 kwanzia 16 Machi 2016 na umekamilika 24 Juni 2018.

Mhe Mabula ameshukuru serikali ya Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Jemedari Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa ushirikiano mkubwa na wadau wa maendeleo kupitia Bank ya Uwekezaji wa watu wa Ulaya EIB  pamoja na Shirika la Maendeleo la France EFB chini ya Usimamizi wa MWAUWASA  kuwezesha kaya 3360 kunufaika. Ikiwa Kaya 2083 kutokea kata ya Mbugani  Mtaa Unguja na wanufaika wanaobaki 1287 ni kutoka Kata ya Igogo Mtaa wa Kwimba kwa gharama za shilingi  1,041,073,366.

Mhe Mabula amesema Mradi huu ni waina yake unaowezesha ujenzi wa Vyoo bora 295 pamoja na utengenezaji wa Mtandao wa Kilometa 5.9 wa mfumo thabiti wa Maji taka ikiwa Kilometa 2.9 Mtaa wa Ugunja Kata ya  Mbugani na Kilometa zilizobakia Kata ya Igogo, kwa Kujenga Chemba 370 zenye uwezo wakuhudumia wakazi 3360 na kusimamiwa na MWAUWASA. Mradi huwa umewezesha kuweka mazingira safi na salama kwa wakazi wa maeneo ya miinuko kwa kudhibiti utapishaji wa vyoo bila kuzingatia misingi ya Afya na kuhatarisha afya kwa uwezekano wa Mlipuko wa magonjwa.

"Nina ipongeza serikali ya awamu ya tano kuzidi  kutekeleza  kwa vitendo uboreshaji wa Mazingira ya watu waishio kwenye miinuko. Halmashauri ya Jiji la Mwanza imezungukwa na Mawe na wakazi wetu wengi wanaishi maeneo ya miiniko, hivyo Kupitia Mradi huu tumeweza kutengeneza njia ya kupita, kadharika na vyoo Bora vyenye uwezo wa kuhifadhi mazingira safi ."  Mhe Mabula Amesema.

Mhe Mabula amemaliza  ziara yake kwa kukutana na vijana na wazee.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: