Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula jana akiwa katika Ziara ya Ukaguzi Miradi ya Maendeleo kata ya Kishiri ameshiriki ujenzi wa Ofisi ya Waalimu ambapo pia kwa kushirikiana na taasis ya First Community Organisation amekabidhi Mifuko ya Saruji kwaajili ya ujenzi wa Ofisi ya Waalimu Shule ya Msingi Kanindo.
Mhe Mabula amesema Mpango wa elimu bure umekuwa na mafanikio makubwa Nyamagana na kuwezesha ongezeko kubwa la idadi ya wanafunzi wanaojiunga na shule ya Msingi na sekondari.
Ametumia adhira hiyo kufafanua kuwa hadi sasa kunauhaba wa madarasa 1000 wilaya ya Nyamagana na serikali katika kipindi hiki kifupi imewezesha ujenzi wa vyumba vya madarasa 100. Mhe Mabula amewaomba wadau wa maendeleo wajitokeze ili kushiriki ujenzi vyumba vya madarasa.
Naye Mwenyekiti wa taasis ya First Community Organisation Ndg Ahmed Misanga amehimiza jamii kuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo ya elimu kwa ujenzi wa madarasa, vyoo pamoja na ofisi za waalimu, Kwani Nyamagana itajengwa na wana Nyamagana.
Wakipokea msaada huo Mwalimu mkuu pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanido wamemshukuru Mhe Mabula kwa mifuko hiyo wanauhakika kukamilisha ujenzi huo kwa wakati. Kadharika wametumia fursa hiyo kumuomba Mhe Mabula pamoja na taasis ya First Community kuwezesha ujenzi wa Madarasa mawili.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Post A Comment: